UFADHILI WA MASOMO YA KOZI ZA UFUNDI 2021

UFADHILI – NAFASI ZA MASOMO – BURE

Chuo cha Ufundi cha Help to Self Help kilichopo SAKINA – JIJINI ARUSHA kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu tunatekeleza programu ya kukuza UJUZI kwa kutoa mafunzo ya ufundi stadi kwa miezi 6 kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 – 35.
Mafunzo haya YANAFADHILIWA na SERIKALI kwa ADA yote kulipwa na SERIKALI KWA ASLIMIA 100.
Fomu zitaanza kutolewa na zitapatikana chuoni HELP TO SELF HELP kuanzia tarehe 19 Aprili hadi 30 Aprili 2021. Masomo yataanza tarehe 17 Mei 2021.

KOZI ZITAKAZOTOLEWA NA SIFA ZAKUJIUNGA

  1. Umeme wa Majumbani
    Sifa: kidato cha nne au zaidi
  2. Upishi
    Sifa: darasa la saba au zaidi
  3. Ushonaji Nguo
    Sifa; darasa la saba au zaidi

Fika chuoni SAKINA – ARUSHA kwa maelezo zaidi

Kwa maelezo zaidi tembelea katika tovuti zifuatazo;
www.kazi.go.tz
www.hsh.or.tz

KWA MAWASILIANO YA KUCHUKUA FOMU – HELP TO SELF HELP VTC
Piga simu zifuatazo;
0744 666 685 au
0744 666 680

 

Email
Facebook
LinkedIn
Twitter

Newsletter

Signup our newsletter